Wakazi wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kuwa makini kutokana na kuwepo kwa vishoka wa wizi wa maji wanaojifanya kuwa ni wafanyakazi wa wizara ya maji chini ya shirika la maji safi na maji taka DAWASCO ambao wamekuwa wakiingia mikataba ya kitapeli na baadhi ya
Kadhia hiyo imemkumba mkazi wa mabibo EXTERNAL Bwana.Saidi Juma ambaye amefungiwa maji kitapeli kutoka mabibo na kijana alifahamika kwa jina la Rajab Mrisho ambaye alimdanganya mzee huyo kuwa ni mfanyakazi wa DAWSCO na kumuunganishia maji hayo kutoka kwenye bomba lingine la mabibo kwa mkataba wa kulipa elfu hamsini kila mwezi.
Waunganishaji wa maji kwa kutumia ujanja ujanja wamekuwa wakirudisha maendeleo nyuma na kuwatia hasara watu wanao waunganishia huduma hiyo bila kibali maalumu ambapo inakuwa ni hatari na hivyo kuchafua jina shirika la maji safi na maji taka DAWASCO nakuonekana kuwa niwalaghai katika utoaji huduma kumbe sio sahihi.







0 comments:
Post a Comment