Msaniii Niki wa Pili ambae anatoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa katika Katiba pendekezwa kidogo anaona inamatumaini kwa upande wa wasaniii maana wameweza kutambulika katika kundi Maalum jambo ambalo litafanya wasaniii na kazi zao kutambulika,lakini katika Katiba ambayo bado inatumiwa wasanii hawajatambulika na hata kazi yao pia jambo ambalo linafanya Niki wa Pili aone kuna afadhali kubwa kwa upande wa wasanii katika katiba pendekezwa.
Niki wa Pili anasema kuwa katiba inayotumiwa sasa Tanzania haitambui kabisa Mali isiyoshikika bali yenyewe inatambua mali inayohamishika kitendo ambacho kinafanya wasaniii mbalimbali wa sanaa kutotambulika na kazi zao hali ambayo inapelekea kundi la wasanii kushindwa kunufaika na kazi za mikono yao.
"katiba tunayotumia inatambua mali inayo hamishika na isiyo hamishika...haitambui mali isiyo shikika sasa huwezi shika formula ya kutengeneza coca, ama pespsi ama dawa ama kinywaji flani lakini ni mali ya mtu....Marekani ili tambua mali isiyo shikika kikatiba toka mwaka 1787...sisi tuko 2015 bado?....ila katika hii katiba pendekezwa naona mwanga flani wasanii wametajwa kama kundi maalumu, pia katika malengo ya kiuchumi ya nchi nadhani na mali isiyo shikika imetajwa....ni hatuwa nzuri"
Lakini pia Niki wa Pili alizidi kufafanua kuwa yeye amezungumzia Katiba pendekezwa kwa kuangalia kundi la wasanii na sii Katiba nzima kiujumla hivyo amewataka vijana,wafanyabiashara,wafanyakazi,Wanafunzi na wananchi kiujumla kila mtu kusoma Katiba pendekezwa kulingana na kundi lao kishawakafanya tafakari kuona kama Katiba hiyo pendekezwa inakidhi haja kulingana na kundi lao hilo,
"vijana wengi mliotowa maoni yenu mko katika makundi either ya wanafunzi,wafanyakazi,ama wafanya biashara.....mimi nimetowa maoni ya kuwa kilisha kundi la wasanii...mnaonaje na nyie wanafunzi, wafanya kazi, wafanya biashara nk mkaisoma na kujuwa imesema nini kuhusu makundi yenu alafu mkafanya tafakari...do ur home work"
Moja ya shabiki wa Niki wa Pili kupitia Ukurasa wa Instgram wa Niki wa Pili alionyesha kukatishwa tamaa na watanzania baada ya kumuelewa tofauti Msanii Niki wa Pili baada ya kuweka matazamo wake juu ya katiba pendekezwa hivyo alikuwa na hili la kusema.
"Hasolin1:Daaah kweli leo nimeamini kiswahili ni kigumu kuliko kiingereza khaaa yaaan Niki wa Pili kashasema yeye hajaongelea katiba in general kaongelea kipengele tu katika hiyo rasimu tena kipengele cha upande wa kazi zake (sanaa) mlivyowaka kama vile @nikkwapili ndio kashapitisha katiba hahahhah tujaribu kuelewa kilichoandikwa kwanza ndio tuchangie narudia tena elewa kwanza ndio uchangie kilichozungumzwa hapa ni kipengele cha wasanii katika rasimu ya katiba na sio kurasmisha katiba na haya ni mawazo yake usimlazimishe afanye unachotaka wewe muache mtu afanye anachotaka na anachofahamu yeye tatizo wabongo sisi wavivu kusoma jaribu kusoma hiyo post hata mara 4 uielewe na ukiilewa naamini hutochangia kinyume na point.







0 comments:
Post a Comment