Comments

Mazishi ya Mbunge wa Jimbo la MBINGA MAGHARIBI Kapteni JOHN KOMBA yanatarajia kufanyika LEO

Mazishi ya Mbunge wa Jimbo la MBINGA MAGHARIBI Kapteni JOHN KOMBA yanatarajia kufanyika LEO Kijijini kwake LITUHI Wilayani NYASA Mkoani RUVUMA.
Mazishi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa huku wengi wakimwelezea Kapteni JOHN KOMBA kuwa kiongozi atakayekumbukwa kwa mchango wake katika kujenga uzalendo. 

Baada ya kuwasili kwa mwili wa Marehemu KOMBA katika Uwanja wa Ndege wa RUHUWIKO ukitokea jijini DSM alipoagwa na Rais , Wabunge na wananchi katika viwanja vya Karimjee, msafara wa mwili wa Kapteni JOHN KOMBA ukaelekea katika Uwanja wa MAJIMAJI ambapo mamia ya wananchi walifurika kuuaga mwili wa mpendwa wao. 

Wananchi na viongozi wa RUVUMA wanasema hawatasahau mchango wa marehemi Kapteni KOMBA katika maendeleo ya Mkoa wa RUVUMA. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amesema shughuli ya mazishi yatakayofanyika Kijijini LITUHI zitaanza Saa TANO Asubuhi pia itahudhuriwa na Rais JAKAYA KIKWETE, viongozi wengine wa Vyama vya Siasa na Serikali. 

Hapo jana marehemu KOMBA aliagwa katika Viwanja vya KARIMJEE Jijini DSM na maelfu ya watu wakiwemo wasanii na wabunge. PAUSE
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos