Comments

Nisher adai Hanscana amegandamizia idea ya video ya Jux kutoka kwenye video ya ‘XO’

Baada ya muimbaji wa R&B Jux kuachia video ya single yake mpya ‘Nikuite Nani’ iliyoongozwa na Hanscana, Nisher amem-mind Hanscana kwa madai kuwa amecopy na kupaste idea ya video hiyo kutoka kwenye video ya ‘XO’ ya Joh Makini.

Nisher ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram alipost picha aliyounganisha screenshot za video ya ‘XO’ ya Joh Makini ambayo aliongoza yeye, pamoja na video mpya ya Jux ‘Nikuite Nani’ iliyoongozwa na Hanscana na kuandika:

“Copy, Paste..Why??? Pesa imekuwa Tamu, IDEA na CONCEPT”


Katika post nyingine Nisher aliweka screeshot ya video ya Young Dee ‘Kijukuu’, pamoja na video ya Y-Tonny ‘Mama’ iliyofanywa na Hanscana na kuandika “Copy, Paste”.


Hata hivyo post hizo tayari zimefutwa kwenye akaunti ya Nisher.

Kama vile haitoshi kwenye akaunti ya ‘bigbrotherafrica_tanzania_fans’ Instagram wamepost picha nyingine yenye video ya zamani ya R.Kelly ‘Fiesta’, ambayo idea yake inafanana na video zote mbili ya Jux na ya Joh Makini.


Wameandika:

Have been to this industry for quite sometime kidogo as an observer lakini…. So nkiona vitu Kama hivi always huwa na’smile tu…. smh
@nisherbybee
@hanscana_

Now I don’t know what Y’all gonna say after seeing this!!!!? Video ya Kwanza chini ni video ya R.Kelly ft Jay Z wimbo Fiesta Fiesta ya zamani… With the same background idea
Video ya pili ya katikati ni ya @joh_makini wimbo wa Xo with the same same Background idea
Video ya juu ni ya @juma_jux wimbo wa Nikuite Nani with the very same background idea

Sasahapa
Nani kuchukua idea ya Mwenzie!? Au wote Sawa!? Anyways Big up to @ommydimpoz Kwa Idea nzuri ya video yako.”


Licha ya kwamba Hanscana hajajibu chochote kuhusu kucopy na kupaste, badala yake ameweka orodha ya video tano zinazofata:

“Five Next Videos are u ready for diamondplatnumz are u ready for mauwa sama n ben pol are u ready for nuh mziwanda are u ready for avid n vanessa mdee are u ready for NAVYKENZO are u ready for Bob jr are u ready for Bele 9 …. Uwiiiiiiiiiiiiii ARE U READY”.



Upande wa Nisher baada ya kuachia video ya Fid Q ‘Bongo Hip Hop’, sasa anatarajia kushoot video ya wimbo wa AY ‘Zigo’ itakayofanyika Zanzibar.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos