Hata hivyo Ommy amesema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.
Ommy ameongea kuwa huenda shughuli nyingi za Diamond ndio sababu iliyomfanya akashindwa kuandika chochote kuhusiana na Wanjera.
“Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”







0 comments:
Post a Comment