Rais JAKAYA KIKWETE amelihutubia Taifa kwa njia ya Televisheni ambapo amezungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwa ni pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Usalama wa Nchi, Mauaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi ALBINO na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa tazama video hapa chini.
Katika hotuba yake hiyo ya kila mwisho wa mwezi Rais KIKWETE amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwani ni fursa pekee ya kupata vitambulisho watakavyotumia katika kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Rais JAKAYA KIKWETE alianza hotuba yake kwa kuipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kazi wanayofanya ya kuandikisha watu kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia mpya ya Kielektroniki -BVR na kutoa wito kwa wananchi kutoungana na wanasiasa wanaopinga uandikishwaji katika daftari hilo.
Pia kiongozi huyu wa TANZANIA akazungumzia kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na kusema kuwa katiba hiyo imetengenezwa na tayari imechapishwa magazetini na kusambazwa kwa wananchi.
Katika hotuba hiyo ya mwezi iliyodumu kwa karibu nusu saa Rais KIKWETE pia alizungumzia mauaji ya ALBINO na kusema serikali itapambana na wote wanaohusika na vitendo hivyo.
Kuhusu usalama wa nchi amesema nchi ipo salama licha ya matukio ya hivi karibuni ya askari kuporwa silaha.







0 comments:
Post a Comment