Vikosi vya uokoaji nchini AFRIKA KUSINI vinapambana kuzima moto wa msituni ulianza kuteketeza misitu ya nchi hiyo tangu jumapili iliyopita.
Maelfu ya ekari za uoto wa asili katika misitu kwenye mbuga za taifa nchini humo yameteketezwa kwa moto. Watu wanaoishi huko CAPE TOWN wameingiwa na hofu kutokana na moto huo wa msituni, ambao hauonyeshi dalili ya kuzimika.
Upepo mkali umekuwa ukiongeza kasi ya moto huo wa msituni. Waokoaji wamekuwa wakitumia helikopta kujaribu kuzima moto huo katika maeneo ambayo magari ya kawaida ya zimamoto yanashindwa kufika.







0 comments:
Post a Comment