Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82 kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali kusababisha mafuriko katika kata ya
mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata ya Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.







0 comments:
Post a Comment