Comments

wapiganaji wa wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini katika mabomu yanayolenga majeshi ya Iraq

Shirika la Utangazaji -BBC- limepata ushahidi unaoonyesha wapiganaji wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini. 

Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq. Serikali ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji Islamic State katika mji wa Tikrit. 

Katika picha video ambayo BBC imeoneshwa na kikosi cha kuharibu mabomu nchini Iraq imeonekana mlipuko wa bomu ukiwa na moshi wa rangi ya chungwa ukipaa angani. Bomu hilo lilikuwa na kiasi kidogo cha Klorini ambayo huenda hutumika kama sumu kwenye maeneo ya wazi. Kumekuwa na taarifa za wapigani wa Islamic State kutumia gesi ya klorini tangu walipoanza harakati zao.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos