Comments

Mbunge wa mbeya joseph mbilinyi (Sugu) anusurika kifo


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amenusu kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la mlima Kitonga mkoani Iringa.

Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake Kwame Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu tumepona.

Amesema pamoja na ajali hiyo kuonekana mbaya kwao, wanamshukuru Mungu kwani waliweza kutoka wakiwa salama na hakuna hata mmoja aliyepata maumivu makali.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos